NAIROBI.Rais Kibaki awashangaza wengi katika hatua yake ya kuwapa tena uwaziri maswahiba zake wawili | Habari za Ulimwengu | DW | 15.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NAIROBI.Rais Kibaki awashangaza wengi katika hatua yake ya kuwapa tena uwaziri maswahiba zake wawili

Rais Mwai Kibaki katika hatua iliyowashangaza wengi amewateuwa tena katika baraza lake la mawaziri wabunge wawili wanao kabiliwa na kashfa za rushwa.

Taarifa ya kitengo cha habari za rais nchini Kenya zimenukuliwa kwamba rais Kibaki amemteuwa George Saitoti kurejelea tena wadhfa wake wa waziri wa elimu na Kiraitu Murungi kuchukuwa tena wadhfa wake wa waziri wa nishati.

Mchambuzi wa maswala ya kisiasa nchini Kenya wakili Patrick Lumumba alikuwa na haya ya kusema.

O ton….Alipofanya uamuzi wa kuwaachisha kwa muda nyadhifa zao za uwaziri bwana Saitoti na bwana Nurungi nilikuwa mmoja wapo aliyetamkja ya kwamba rais Kibaki hakufanya uamuzi wa kuwapiga kalamu jkabisa kili ambcho alifanya li kuwapa vyombo na taasisi za kitaifa zichunguze madai dhidi ya Saitoti na Kiraitu kwa hivyo mimi sikushangazwa kwa yeye kuwatudisha tena kwani hao ni wapambe wake na hasa uchaguzi mkuu wa mwaka ujaoi ukiwa karibu…

Mawaziri hao walijiuzulu mwezi Februari kufuatia shinikizo kwa rais Kibaki lililomtaka achukue hatua dhidi ya mawaziri wake walio husishwa na kashfa za rushwa.

Saitoti anatuhumiwa kuhusika na kashfa kubwa ya rushwa ya mwaka 1990 wakati alipokuwa makamu wa rais kwenye utawala wa rais mstaafu Daniel Arap Moi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com