NAIROBI:Meli ya Taiwan iliyotekwa yawasili Maombasa kwa ukarabati | Habari za Ulimwengu | DW | 14.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NAIROBI:Meli ya Taiwan iliyotekwa yawasili Maombasa kwa ukarabati

Meli moja ya Taiwan iliyoachiwa na maharamia wa Kisomali wiki jana imewasili mjini Mombasa hii leo ili kufanyiwa ukarabati.

Ching Fong Hwa 168 pamoja na wafanyikazi wake wawili raia wa Taiwan na 14 wa Kichina waliachiwa tarehe 5 mwezi huu baada ya kuzuiliwa kwa zaidi ya miezi mitano.

Maharamia hao walimuua mmoja ya wafanyikazi hao baada ya mwenye meli kukataa kutimiza madai yao ya pesa za kukomboa mateka hao.

Nchi ya Somali iko kwenye mdomo wa Bahari ya Sham ambalo ni eneo kuu la biashara kati ya Bara Asia na Ulaya kupitia mfereji wa Suez.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com