NAIROBI:Mabaki ya ndege ya kenya yagunduliwa | Habari za Ulimwengu | DW | 07.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

NAIROBI:Mabaki ya ndege ya kenya yagunduliwa

Maafisa wa safari za ndege wa Kenya wamesema kundi linaloendesha shughuli za uokoaji limegundua mabaki ya ndege ya shirika la ndege la Kenya iliyoanguka jumamosi kusini mwa Cameroon ikiwa na watu 114.

Mabaki hayo ya ndege yameonekana kwenye sehemu yenye majimaji kiasi kilomita 20 kutoka uwanja wa ndege wa Douala kusini mwa Cameroun.

Hata hivyo hadi sasa bado hakuna taarifa zozote zilizotolewa kuhusu uwezekano wa kuwepo manusura.

Ndege hiyo aina ya Boeing 737-800 ilipoteza mawasiliano muda mfupi baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Douala.Ndege hiyo ilianza safari yake kutoka Abidjan Ivory Coast,uwanja wa Ndege wa Douala ilikuwa kituo chake cha Pili kuelekea Nairobi Kenya.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com