1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Mwanadiplomasia wa Ufaransa anatarajiwa kuitembelea China

29 Machi 2024

Msemaji wa wizara ya kigeni ya China Lin Jian amesema Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Stephane Sejourne anatarajiwa kufanya ziara nchini China siku ya Jumatatu.

https://p.dw.com/p/4eG91
Ufaransa na China zaadhimisha miaka 60 ya uhusiano wao
Ufaransa na China zaadhimisha miaka 60 ya uhusiano waoPicha: Sarah Meyssonnier/REUTERS

Ufaransa na China zimekuwa zikitaka kuendeleza mahusiano yao katika miaka ya hivi karibuni na katika mikutano iliyofanyika mjini Paris mwezi uliopita, Wang Yi Waziri wa mambo ya nje wa China alimwambia rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwamba Beijing inathamini msimamo wa Ufaransa wa kujitegemea.

Macro aliitembelea China mwezi Aprili mwaka uliopita katika ziara iliyokuwa na mashaka baada ya rais huyo wa Ufaransa kuonekana kujisogeza karibu na China wakati aliposema kwamba Ulaya hailazimiki kufuata msimamo wa Marekani linapokuja suala la mgogoro wa China na Taiwan.