Mwalimu wa Uingereza ahukumiwa kifungo cha siku 15 | Habari za Ulimwengu | DW | 30.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Mwalimu wa Uingereza ahukumiwa kifungo cha siku 15

Mahkama nchini Sudan imemuona mwalimu wa Uingereza kuwa na hatia ya kuwatukana Waislamu kwa kuliruhusu darasa lake kumwita dubu wa kuchezea jina la Muhammad ambalo ni jina la mtume wa Waislamu.

Gillian Gibbons amehukumiwa kifungo cha siku kumi na tano gerezani na baadae atarudishwa kwao Uingereza. Mjini London waziri wa mambo ya nje wa Uingereza David Miliband amesema amevunjwa moyo sana na hukumu hiyo na amemwita balozi wa Sudan nchini humo kwa ajili ya kutowa ufafanuzi.

Gibbons ameepuka kushtakiwa kuchochea chuki na kuonyesha dharao kwa imani za dini.

Mmojawapo wa mawakili wanaomtetea ames ema atakata rufaa kupinga hukumu hiyo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com