1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mvutano bomba la mafuta la Druzhba wazidi makali

6 Machi 2026

Hungary imesema itazuia usafirishaji wa bidhaa zote muhimu kwenda Ukraine hadi pale mafuta kutoka Urusi yakapoanza kusafirishwa tena kuingia Hungary kupitia bomba linalokatisha ndani ya Ukraine.

https://p.dw.com/p/59uZS
Bomba la mafuta la Druzhba
Ukraine inasema bomba la Druzhba limeharibiwa na mashambulizi ya Urusi.Picha: Bernadett Szabo/REUTERS

Waziri Mkuu wa Hungary Victor Orban amekiambia kituo cha redio ya taifa leo Ijumaa, kuwa serikali mjini Budapest imekwishazuia upelekaji mafuta ya diesel nchini Ukraine na kwamba imedhamiria kuzuia bidhaa zote kupelekwa nchini humo mpaka bomba la mafuta la Druzhba litakapoanza tena kufanya kazi.

Kusimama kwa usafirishaji mafuta kupitia bomba la Druzhba kumekuwa chanzo cha mvutano mkubwa kati ya Ukraine na Hungary pamoja na Slovakia.

Ukraine imesema limeharibiwa na mashambulizi ya Urusi na inafanya jitihada zote kulikarabati. Hata hivyo, Hungary na Slovakia zimeishutumu Ukraine kufanya kazi hiyo kwa kasi ya kujikokota.