1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MUWAZA/Jumuiya ya Wazanzibari walio ngambo

Othman, Miraji8 Septemba 2008

Muwaza; Jumuiya ya Wazanzibari wanaotaka mustakbali mpya wa Visiwa vyao

https://p.dw.com/p/FDYi
Mji mkongwe wa ZanzibarPicha: DW /Maya Dreyer

Karibuni kumeundwa Jumuiya ya Wazanzibari wanaoishi ngambo kwa jina la MUWAZA, yaani Mustakbali Wa Zanzibar. Kwa mujibu wa waasisi wake, malengo ya jumuiya hiyo ni kuwaunganisha Wazanzibari wote ili kuleta utambulisho wa Wa-Zanzibari na kuleta suluhu baina yao na kupigania mustakbali wa Zanzibar kama nchi, kwa ujumla, na kulinda maslahi ya kidola, kitaifa na kulinda uhuru wake.


Kwa ajili ya kipindi hiki cha Mapambazuko Afrika, kinachowajia kila wiki saa kama hizi, kutoka Deutsche Welle, Bonn, Othman Miraji alizungumza kwa njia ya simu na kiongozi wa waasisi wa jumuiya hiyo, Dr. Yusuf Saleh Salim, aliyoko katika mji mkuu wa Denmark, Copenhage. Kwanza nilitaka kujuwa kitu gani kilichowachochea kuanzisha jumuiya hiyo, tena wakati huu....