Moscow. Shauri la upelelezi juu ya kifo cha Litvinenko lazua mzozo wa kidiplomasia. | Habari za Ulimwengu | DW | 05.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Moscow. Shauri la upelelezi juu ya kifo cha Litvinenko lazua mzozo wa kidiplomasia.

Wapelelezi wa Uingereza wako nchini Moscow kuendelea na uchunguzi wao katika kifo kutokana na kupewa sumu ya miale kwa jasusi wa zamani wa Urusi Alexander Litvinenko.

Maafisa hao walikuwa wanatarajiwa kuwahoji watu watatu raia wa Urusi ambao walikutana na Litvinenko Novemba mosi, siku ambayo alianza kuugua.

Kuwasili kwa wapelelezi hao mjini Moscow kumesababisha mzozo wa kidiplomasia baina ya Urusi na Uingereza.

Gazeti la Times limeripoti leo kuwa maafisa hao wa upelelezi wa Uingereza wanahakika kuwa majasusi wa kitengo cha ujasusi cha Urusi wameidhinisha mauaji hayo.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergey Lavrov amesema kuwa mashauri hayo yanaathiri mahusiano kati ya nchi hizo mbili. Urusi imekana kuhusika na mauaji ya Litvinenko, ambaye alikuwa mkosoaji mkubwa wa rais wa Urusi Vladimir Putin.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com