MOSCOW : Kifo cha Litvinenko ni mauaji | Habari za Ulimwengu | DW | 07.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOSCOW : Kifo cha Litvinenko ni mauaji

Polisi ya Uingereza imesema hivi sasa wanakiona kifo kutokana na kupewa sumu cha mpelelezi wa zamani wa Urusi Alexander Litvinenko kuwa ni mauaji.

Litvinenko ambaye alikuwa mkosoaji mkali wa Rais Vladimir Putin wa Urusi amekufa mjini London wiki tatu zilizopita.Kabla ya kifo chake Litvinenko alimshutumu Putin kwa kuamuru kuuwawa kwake.

Mjini Moscow polisi ya Uingereza na wapelelezi kutoka ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa serikali walimhoji Dmitry Kovtun mlinzi wa zamani wa shirika la ujasusi la Urusi KGB ambaye ni mmojawapo ya Warusi wawili ambao walikutana na mpelelezi huyo wa zamani hapo Novemba Mosi siku ambayo Litvinenko aliuguwa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com