MONROVIA :Marais Hu na Sirleaf watia saini mikataba ya biashara | Habari za Ulimwengu | DW | 02.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MONROVIA :Marais Hu na Sirleaf watia saini mikataba ya biashara

Rais Hu Jintao wa China ameizuru Liberia-kituo cha pili cha ziara yake katika nchi nane barani Afrika.Kiongozi huyo wa China alikuwa na mazungumzo pamoja na rais wa Liberia Bi.Ellen Johnson Sirleaf.Viongozi hao wametia saini makubaliano ya pande mbili kuhusika na sekta za biashara,elimu na afya.Sudan,iliyo na utajiri wa mafuta,ni kituo kingine katika ziara ya rais Hu anaekabiliwa na shinikizo la kimataifa kutumia ushawishi wa China kumaliza mgogoro wa Darfur uliosababisha vifo vya zaidi ya watu 200,000 katika kipindi cha miaka minne.Inaaminiwa kuwa Beijing kama mwekezaji mkuu kabisa wa kigeni nchini Sudan,ina uwezo wa kuishawishi serikali ya Khartoum kuruhusu vikosi vya amani vya Umoja wa Mataifa kupelekwa Darfur.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com