MOGADISHU: Majeshi ya serikali yateka ngome ya mwisho ya wanamgambo nchini Somalia. | Habari za Ulimwengu | DW | 13.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MOGADISHU: Majeshi ya serikali yateka ngome ya mwisho ya wanamgambo nchini Somalia.

Majeshi ya serikali ya Somalia, yanayosaidiwa na Ethiopia, yamesema yameteka ngome ya mwisho ya wanamgambo wa Kiislamu kusini mwa nchi hiyo.

Msemaji wa serikali amesema majeshi yamekiteka kijiji cha pwani cha Ras Kamboni ambako wanamgambo wa Kiislamu walikimbilia.

Taarifa zinasema wanamgambo wengi wamekamatwa.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com