Mjadala katika chama cha CDU, Merkel ageukia mrengo wa kati | Matukio ya Kisiasa | DW | 14.09.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Mjadala katika chama cha CDU, Merkel ageukia mrengo wa kati

Nini kinaweza kutokea katika sura ya vyama iwapo vyama vyote vitajiweka katika nadharia ya mrengo wa kati kisiasa, ni maadili gani ambayo chama kitapaswa kuyakumbatia?

Kansela wa Ujerumani na kiongozi wa chama cha CDU Angela Merkel.

Kansela wa Ujerumani na kiongozi wa chama cha CDU Angela Merkel.

Jee Iwapo vyama vyote vitajiweka katika nadharia za mrengo wa kati kisiasa , nini kitatokea katika sura za vyama. Ni maadili gani ambayo chama kitapaswa kuwa nayo ?-Kama ni chama cha wananchi. Maswali haya yanajitokeza kwa nguvu na mtazamo mpya katika utaratibu wa chama cha CDU na hali hiyo imezushwa na hasira baada ya rais wa muungano wa vyama hivyo Erika Steinbach kupata matatizo katika chama hicho, pamoja na mjadala mpya juu ya ujumuisho wa wageni nchini Ujerumani.

Ni kundi dogo la waandamanaji , ambalo limeamua kuandamana mbele ya makao makuu ya chama cha CDU mjini Berlin. Wameweka bango moja kubwa, ambalo linatahadharisha , kwamba msimamo wa Kikristo katika chama hicho unapotea. Hawa ni wanachama wa tawi la vijana wa chama hicho kutoka katika eneo la Ruhr. Mmojawao , Jacek Spendel , amesema.

Ujumbe wa Kikristo , maadili ya Kikristo, mtazamo wa Kikristo, hautiliwi maanani. Sioni tofauti tena kati ya chama cha SPD ama hata FDP, vyote ni sawa tu, na nadhani , hali hii haiwezi kuendelea hivyo. Ama viongozi kule juu waamke, ama tunapaswa kufikiria upya kile tunachoweza kufanya, kwamba tuanzishe chama chetu kipya.

Mawazo haya yanakutikana kwa hivi sasa kwa wengi wa wanachama wa CDU. Si mara ya kwanza , lakini tangu pale Angela Merkel aliposhika madaraka ya chama hicho na kukipeleka chama hicho katika nadharia ya mrengo wa kati, mtazamo huo umeanza kupata nguvu zaidi. Angela Merkel anatetea mradi wake huo, na kuwezesha kundi la wanasiasa wengi kuunga mkono mtazamo wake.

Nataka kusisitiza kwa mara nyingine , kwamba hiki ni chama chenye mizizi kutoka sehemu tatu, Kiliberali, jamii ya Kikristo na kihafidhina. Hakuna hata sehemu moja kati ya hizi ambazo kwetu sisi si muhimu , badala yake sehemu zote tatu zinatoa nguvu kwa chama hiki kuwa chama cha wananchi. Na pia naona moja ya kazi za CDU, ni kuangalia kuwa , hakuna chama ambacho kinaelemea katika imani kali.

Njia ya kuelekea msimamo wa kati wa kansela Merkel unakipeleka chama katika hali ya kutatanisha na yenye maumivu. Maadili ya kiutamaduni yaliyozoeleka hayaangaliwi na wapiga kura , ambao ni wahafidhina, wa mrengo wa kulia ama Wakristo, wanataka kuendelea kuuchukua utamaduni huo kwenda nao katika chama kipya. Hilo si rahisi, na kutokana na kufutwa kwa mfumo wa vijana kutumikia jeshini kwa muda kwa mujibu wa sheria, hilo limewakasirisha wahafidhina. Kuna mjadala mpya kuhusu kujumuishwa kwa wageni nchini humu, ambamo kuna ishara za chuki dhidi ya wageni ambazo inaonekana zinawakera viongozi wa juu wa chama hicho, lakini zinakwenda sawa na mtazamo wa wapiga kura. Pia kuna hasira dhidi ya kufukuzwa kwa rais wa muungano wa vyama hivyo vya kihafidhina Erika Steinbach, mwanamke maarufu katika muungano huo, ambaye wanamtetea kuhusiana na matamshi yake kuhusiana na fedha zinazotumika katika vita. Kutokana na hali hiyo idadi kubwa ya wapiga kura wa CDU sasa inapungua.

Mwandishi Kiesel, Heiner / ZR / Sekione Kitojo

Mhariri : Mohammed Abdul Rahman

 • Tarehe 14.09.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/PBlX
 • Tarehe 14.09.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/PBlX
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com