Misimamo ya Wajerumani wa Magharibi na wa Mashariki bado inatofautiana | Matukio ya Kisiasa | DW | 06.11.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Miaka 30 baada ya kuporomoshwa kwa ukuta wa Berlin

Misimamo ya Wajerumani wa Magharibi na wa Mashariki bado inatofautiana

Uchambuzi: Miaka 30 tangu Ujerumani zilipoungana tena watu wanajiuliza kwanini misimamo ya Wajerumani wa eneo la Magharibi na wale wa eneo la Mashariki ingali bado inatofautiana?

Eneo la Mashariki linaimarika vyema kiuchumi. Hayo ndio matokeo ya ripoti ya serikali kuu ya Ujerumani iliyochapishwa hivi karibuni kuhusu "Hali ya Muungano wa Ujerumani." "Kukuwa pamoja Ujerumani na kuhakikisha usawa katika hali ya maisha ni mambo yaliyofana kwa sehemu kubwa hadi sasa". Kisiasa na nyoyoni mwa watu lakini bado mtengano unaonyesha ni mkubwa.  Utafiti wa maoni umebainisha asili mia 57 ya wakaazi wa Ujerumani Mashariki wanajihisi kuwa ni watu wa daraja la pili na takriban nusu kati yao hawaridhiki na jinsi mfumo wa demokrasia unavyoendeshwa. Pengo ni pana zaidi kati ya wakaazi wa Mashariki na wale wa Magharibi linapozuka suala la kutathmini upya muungano. 

Mtaalam wa saikolojia kutoka mashariki mwa Ujerumani Hans-Joachim Maaz anahisi Wajerumani Mashariki kutokana na maarifa waliyojikusanyia katika enzi za GDR, hawakuwa na uhusiano na serikali. "Wakaazi wa Mashariki kwa jumla ni wenye kupinga ubepari" wanapinga uongozi na ni wenye kukosoa vyombo vya habari pia. Ndio maana kuna wimbi la malalamiko dhidi ya sera za Ujerumani magharibi za kutaka kudhibiti kila kitu."

Deutschland Mauerfall Grenzöffnung Berlin Trabi vor Grenzübergang (imago/Sven Simon)

Furaha iliyopatikana 1989 haipo tena

Mtaalam wa saikolojia ya jamii kutoka Ujerumani Magharibi Beate Küpper ana maoni tofauti na hayo anasema kwa upande wake kwamba kutokana na kutenganishwa na ukuta kwa muda mrefu ndio maana si jambo la kushangaza kuona kwamba Wajerumani Mashariki na wale wa Magharibi hawana msimamo wa aina moja. Tatizo sio tofauti iliyoko bali hisia jumla za watu kuamini hawatendewi sawa."Ni suala la hisia za kutambulika, kuthaminiwa, na kuwa na usemi."

Pengine mfano dhahiri zaidi unakutikana katika matokeo ya uchaguzi ya chama cha siasa kali za mrengo wa kulia "Chaguo Mbadala kwa Ujerumani" AfD. Katika chaguzi za majimbo katika maeneo ya magharibi chama hicho hujikingia kiwango cha karibu asili mia 10, katika maeneo ya mashariki wanajipatia asili mia 25 ya kura kama ilivyoshuhudiwa hivi karibuni katika majimbo ya Brandenburg, Saxony na Thüringia.

Landtagswahl Brandenburg AFD Wahlplakat (Reuters/H. Hanschke)

Bango la kampeni la chama cha AfD

Katika eneo la Mashariki AfD kimechukua nafasi ya chama cha malalamiko cha "die Linke" ambacho ni chimbuko la chama tawala katika ile iliyokuwa zamani ikijulikana kama GDR-SED katika kupalilia hisia na hamu ya yale waliyokuwa nayo upande wa mashariki. Katika kampeni za uchaguzi, upande wa mashariki kauli mbiu ya chama cha AfD ilikuwa :"Tukamilishe mageuzi". Na wamefanikiwa. Mtaalam wa saikolojia Hans Joachim Maaz anahisi ni kosa kubwa kuwapiga mhuri wa siasa kali za mrengo wakulia wale waliokipigia kura chama cha AfD katika majimbo ya mashariki. Wanapokaripiwa na kubaguliwa ndipo nacho chama cha AfD kinapozidi kupata nguvu, anasema.

 

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com