1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Jordanien König Abdullah II
Picha: Getty Images/AFP/K. Mazraawi

Mipango ya Trump kuigeuza Jordan kuwa taifa la Palestina

Sylvia Mwehozi
14 Juni 2019

Mfalme Abdullah wa Jordan amekosoa vikali pendekezo lolote la kwamba anaweza kukubaliana na mpango wa Marekani wa kumaliza mgogoro wa siku nyingi wa Israel kwa kuwakaribisha Wapalestina ndani ya taifa lake.

https://p.dw.com/p/3KTZ9

Wakati alipovihutubia vikosi vya usalama mwezi Machi, Mfalme huyo alikataa wazo la kwamba Jordan inaweza kuwa ni mbadala wa taifa la Wapalestina, akihoji je taifa hilo halina sauti?

Baada ya kuundwa kwa taifa la Israel mwaka 1948, Jordan iliwapokea Wapalestina wengi kuliko nchi nyingine, ambapo sasa inakadiriwa kuwa huenda wanafikia nusu ya idadi ya wakaazi wote. Ahadi ya muda mrefu ya Rais wa Marekani Donald Trump ya kuutafutia ufumbuzi mgogoro wa karne bado imekuwa siri, ingawa taarifa zilizovuja zinapendekeza wazo la taifa kamili la kipalestina kwa kuzingatia sehemu tu utawala binafsi katika maeneo yaliyokaliwa suala linalotajwa kuwa litadhoofisha haki ya Wapalestina kurejea.

Inataja juu ya upanuzi wa Gaza hadi maeneo ya kaskazini mwa Misri chini ya utawala wa nchi hiyo huku pia Wapalestina wakiwa na haki kidogo katika ukingo wa Magharibi na baadhi ya maeneo nje ya Jerusalem bila ya kuwa na udhibiti wa mipaka yake.

Jordanien | Trump-Berater Jared Kushner reist in den Nahen Osten
Mshauri wa White House Jared Kushner na Mfalme Abdullah Picha: Reuters//Royal Palace/Y. Allan

Idadi ya Wapalestina nchini Jordan

Wajordani wanahofu juu ya raia walio na asili ya Kipalestina na kwa ajili ya siasa za ndani kwamba vyote hivyo vimechochewa na utayari wa Trump wa kubadili sera ya Marekani. Maafisa wa Marekani hata hivyo wanakataa wazo la kuifanya Jordan kuwa taifa la Wapalestina. Lakini mbinu chafu za Trump kuhusiana na suala hilo na kauli za hivi karibuni za balozi wake nchini Israel kwamba ina haki ya kupora maeneo zaidi ukingo wa magharibi, vyote hivyo haviwezi kutuliza wasiwasi wa Jordan.

Uwepo wa Wapalestina nchini Jordan ni suala ambalo lina unyeti wa kisiasa. Hakuna data rasmi za Wapalestina wangapi wapo nchini Jordan , nchi iliyo na wakazi milioni 8. Licha ya Marekani kukataa mpango huo, Wajordan wanahofu kuwa Trump anarejea katika wimbo wa siku zote kwamba Jordan ni Palestina na kwamba hapo ndipo Wapalestina walioko ukingo wa magharibi wanakotakiwa kwenda.

Suala hilo linakuja wakati mbaya ambao Mfalme Abdullah anatimiza miaka 57 na ambaye nchi yake inakabiliwa na changamoto za kiuchumi ambazo zimesababisha maandamano na kubadilishwa kwa serikali mwaka jana. Wakati Wapalestina wengi wakiwa wamechangamana vyema nchini Jordan, wengi hawajawahi kutia mguu katika ardhi yao ya asili. Hofu kubwa ni kwamba mipango ya Trump itaingilia demografia na siasa za ndani  zinazoathiriwa na uwepo wa Wapalestina, ambao wana uraia kamilifu lakini wametengwa kwasababu wanaonekana kama kitisho cha kisiasa dhidi ya Wajordan wenyewe.

Saudi Arabien König Salman bin Abdulaziz in Tunis
Mfalme Abdullah akihudhuria mkutano wa nchi za Kiarabu TunisiaPicha: picture-alliance/AP Photo/F. Belaid

Kudumisha mshikamano baina ya raia wa Jordan na walio na asili ya Palestina, limekuwa ni jambo muhimu sana katika utawala wa familia ya Kifalme. Mfalme tayari anakabiliwa na hasira kutoka kwa upinzani "Herak" ambao ni wa asili ya Jordan wakisema kwamba mipango ya Trump itauvuruga mfumo wa usimamizi ambao umedumisha utiifu kwa ufalme. Soma zaidi...

Wengi wameonya utawala wa kifalme kutokubaliana na mpango huo wa Trump kwasababu utawapatia haki zaidi za kisisasa wapalestina katika mfumo wa uchaguzi ambao unawapendelea raia wazawa. Tetesi kwamba mpango huo utasababisha Jordan kuwapokea wakimbizi zaidi wa Kipalestina kutoka Lebanon na Syria umetoa wasiwasi zaidi. "Trump anataka kuinunua na kuiuza Jordan na kutengeneza utawala mpya", alisema Muraed al-Adaylah, mkuu wa kituo cha udugu wa Kiislam.

shinikizo la nje

Mkakati wa muda mrefu wa Jordan na sera za kiuchumi zimesimama katika mahusiano ya karibu ya nchi za magharibi na matifa ya Ghuba, mbinu iliyochangia maamuzi yake kufanya amani na Israel mwaka 1994. Abdullah amekuwa na ziara chungu nzima nchini Marekani, ambako maafisa wanasema hakupewa maelezo juu ya mpango wa Trump. Wachambuzi, baadhi yao wanadhani kuwa Jordan ambayo inakabiliwa na changamoto za kiuchumi inaweza kunufaika na mpango wowote ambao utaahidi mabilioni ya misaada na ufadhili wa miradi. reuters