1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MILAN:Mmisri aliyehusika na mashambulio ya Madrid kufungwa jela miaka 10

7 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCvM

Makahama ya Italia imemhukumu kifungo cha miaka 10 jela mtuhumiwa mkuu wa mashambulio ya mabomu yaliyotokea kwenye kituo cha treni mjini Madrid mwaka 2004.

Washataki wa Milan walitaka raia huyo wa Misri Rabei Osman Sayed Ahmed mwenye umri wa miaka 35 ahukumiwe kifungo cha miaka 14 jela wakisema anamafungamano na mtandao wa kigaidi ulioenea kote barani ulaya.

Mtuhumiwa mwingine aliyekuwa akizuiliwa amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela.

Mmisri Rabei Ahmed ambaye alikamatwa mjini Milan miezi mitatu baada ya mashmbulio ya Madrid amekanusha kuwa na mafungamano na kundi la itikadi kadi za kiislamu la nchini Misri.

Rabei anatazamiwa kurudishwa nchini Uhispania atakakoshtakiwa pamoja na washukiwa wengine 20 wa mashambulio ya madrid mapema mwakani.

Watu 191 waliuwawa na wengi kujeruhiwa kwenye mashambulio hayo dhidi ya treni mjini Madrid mwaka 2004.