Mikutano ya Hali ya Hewa Marekani Juma hili. | Masuala ya Jamii | DW | 21.09.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Masuala ya Jamii

Mikutano ya Hali ya Hewa Marekani Juma hili.

Wawakilishi kutoka kote duniani wanakusanyika nchini Marekani kwa mazungumzo ya wiki moja kuhusu hali ya hewa duniani. Leo Katibu mkuu wa umoja wa mataifa anaandaa mkutano wake binafsi wa hali ya hewa.

default

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon.

Mikutano hiyo ya karibuni kabisa katika mlolongo wa mikutano rasmi na isiyo rasmi, itawapa fursa viongozi awa kimataifa kubadilishana mawazo jinsi ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa kabla ya mkutano wa umoja wa mataifa juu ya hali ya hewa mjini Copenhagen mwezi Desemba.

Mhadhiri katika chuo kikuu huria cha Berlin Profesa Miranda Schreurs ambaye pia ni mjumbe katika halmashauri ya Ujerumani ya ushauri juu ya mazingira anasema kuna mikutano zaidi na zaidi ya mazingira ambayo inazidi kuwa ya utata na inayoongeza masuala zaidi ya kujadiliwa. Inaweza kuwa ni mzigo kawa umma na pia wajumbe wanaofanya kazi siku nzima na kusafiri kutoka mkutano mmoja hadi mwengine.

Kile kinachojulikana kama wiki ya hali ya hewa kinaanza na mkutano wa Alahamisi iliopita mjini Washington na kuendelea katika makao makuu aya umoja wa mataiafa mjini New york na kumalizikia na mkutano wa viongozi wa kundi la G20 watakaokutana huko Pittsburgh kwa mazungumzo ya siku mbili kuanzia Alhamisi ijayo.

Sekretariati ya mazingira ya Umoja wa mataifa UNFCCC itakua na mazungumzo mjini Bangkok na Barcelona kabla ya mkutano wa Copenhagen nchini Denmark.Kim Carstensen mkuu wa kundi linalopigia debe hifadhi ya mazingira duniani anasema hiyo itakua nafasi nzuri ya kuonyesha nia ya kisiasa kukabiliana na ongezeko la ujoto duniani.

Lengo la umoja wa mataifa ni kuwakusanya mawaziri wa mazingira watakaokutana Copenhagen mwezi Desemba kukubaliana kuwa na duru mpya ya mazungumzo kuhusu upunguzaji viwango vya utoaji gesi zinazoharibu mazingira, jambo litakaloanza kutekelezwa baada ya kumalizika mkataba wa Kyoto 2012. Lakini hadi asasa makubaliano kama hayo yako mbali na kufikiwa.

Mazungumzo yanayoendelea yamekwama kwa miezi kadhaa sasa, kwa sababu ya nchi za viwanda kukataa kutoa mchango wa haki kulinda mazingira duniani.

Katibu mkuu wa umoja wa mataiafa amekua akionya kwamba mabadiliko ya hali ya hewa yatakua na athari kubwa kwa sayari nzima ya dunia ikiwa viongozi watashindwa kufikia maridhiano juu ya suala hilo.

Licha ya kuwepo kwa mkataba wa Kyoto ana juhudi za nchi moaja moja, utoaji wa hewa ya carbon dioxide inayoharibu mazingira umeongezeka kwa asili mia 30 tangu 1990 na kwa mujibu wa Profesa Schreurs wa chuo kikuu huria cha Berlin nchi zilizo mstari wa mbele hazina budi kuzishinikiza nyengine kuchukua hatua.

Kwa mujibu wa mhadhiri huyo, baadhi aya wakati watu wanaweza kufikia mwafaka kuhusu bia abaada ya siku kadhaa za majadiliano au wajumbe wanapokutana kawa mahati kwenye viwanja vya ndege, lakini wanashindwa kuona umuhimu wa kufikia makubaliano juu ya suala hili la hali ya hewa, ambalo ni kitisho kikubwa kwa binaadamu. pamoja na hayo bado bibi Schreurs anatumai makubaliano yatakayojumuisha pia suala la viwango vya utoaji wa hewa chafu zinazoharibu mazingira hadi 2050, yataweza kufikiwa katika wakati uliokusudiwa na kutiwa saini wakati wa mkutano ujao wa Copenhagen.

Mwandishi: Sinico Sean/ DW Online/

Abdul-Rahman/Mzurikwao

Mhariri: Othman Miraji

 • Tarehe 21.09.2009
 • Mwandishi Halima Nyanza
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Jlog
 • Tarehe 21.09.2009
 • Mwandishi Halima Nyanza
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/Jlog
Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com