1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Mike Pence asema hatomuunga mkono Trump kwenye uchaguzi

16 Machi 2024

Makamu wa Rais wa zamani wa Marekani Mike Pence amesema hatomuunga mkono Donald Trump katika uchaguzi wa mwaka huu.

https://p.dw.com/p/4dnez
Makamu wa Rais wa zamani wa Marekani Mike Pence
Makamu wa Rais wa zamani wa Marekani Mike PencePicha: Susan Walsh/AP/dpa/picture alliance

Pence amesema hayo katika mahojiano na kituo cha habari cha Fox ambapo ametoa kauli hiyo nzito kwa mara ya kwanza tangu ionekane wazi kwamba Trump atakuwa mgombea urais wa chama cha Republican.

Wajumbe na maafisa wengine wa chama cha Republican wameungana kwa kiasi kikubwa kumuunga mkono Donald Trump, ingawa wachache wenye uzito kwenye chama hicho wameendelea kumpinga.

Soma pia: Pence awasilisha nyaraka za kuwania urais 2024

Mike Pence alikuwa ni mmoja wa watetezi waaminifu zaidi wa Donald Trump lakini alijitenga na rais huyo wa zamani kwa kukataa kuunga mkono mpango wa Trump uliokiuka katiba pale alipojaribu kubaki madarakani baada ya kushindwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2020.