MEXICO CITY: Rais Bush aendelea na ziara yake ya Amerika ya Kusini | Habari za Ulimwengu | DW | 13.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

MEXICO CITY: Rais Bush aendelea na ziara yake ya Amerika ya Kusini

Rais George W Bush wa Marekani yumo nchini Mexico katika awamu ya mwisho ya ziara yake ya wiki moja ya Amerika ya Kusini. Rais Bush anatarajiwa kukutana na rais wa Mexico, Felipe Calderon, kuzungumzia maswala nyeti kama vile uhamiaji, kudhibiti eneo la mpakani na biashara haramu ya dawa za kulevya.

Maandamano yamekuwa yakifanywa kila mahali rais Bush alipotembelea na rais wa Venezuela Hugo Chavez amemshambulia vikali kiongozi huyo.

Rais Chavez amezuru eneo hilo sambamba na ziara ya rais Bush kuzungumzia dhidi ya kile anachokiita kuingiliwa kwa ufalme wa Marekani.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com