1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merz hakati tamaa kuhusu uhusiano wa Ujerumani na Marekani

4 Mei 2026

Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz amesema hakati tamaa kuhusu uhusiano wa Ujerumani na Marekani na kushirikiana na rais wa Marekani Donald Trump. Katika mahojiano na kituo cha utangazaji cha Ujerumani, ARD, Jumapili.

https://p.dw.com/p/5DC2q
Kansela Friedrich Merz alikiri kwamba yeye na Trump wana mitazamo tofauti kuhusu vita vya Iran, lakini alipuuza ugomvi wao wa hadharani
Kansela Friedrich Merz alikiri kwamba yeye na Trump wana mitazamo tofauti kuhusu vita vya Iran, lakini alipuuza ugomvi wao wa hadharaniPicha: Thomas Ernst/ARD/dts Nachrichtenagentur/IMAGO

Kansela wa Ujerumani Friedrich Merzamesema hakati tamaa kuhusu uhusiano wa Ujerumani na Marekani na kushirikiana na rais wa Marekani Donald Trump.Katika mahojiano na kituo cha utangazaji cha Ujerumani, ARD, jana Jumapili Merz alisema hakukuwa na uhusiano kati ya yeye kutokubaliana na Trump kuhusu vita vya Iran, na kuondolewa kwa wanajeshi wa Marekani kutoka Ujerumani.

Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz alizungumzia hali ya uhusiano wa pande mbili na Marekani kufuatia ugomvi wa hadharani kati yake na rais wa Marekani Donald Trump kuhusu vita nchini Iran.

Katika mahojiano na kituo cha utangazaji cha umma cha UjerumaniARD, Merz alipunguza mvutano kati ya nchi hizo mbili. Alisema kwamba tangazo la Trump la kuondoa wanajeshi 5,000 wa Marekani kutoka kambi za kijeshi nchini Ujerumani halikushangaza na halitaonekana kama kulipiza kisasi, akiongeza kuwa halina uhusiano na yeye kutokubaliana na Trump katiaks siku chache zilizopita.

Merz alisema nini kuhusu uhusiano wa nchi za Ulaya na Marekani?

Merz alisema hakati tamaa kufanya kazi katika uhusiano wa nchi za Ulaya na Marekani wala hakati tamaa kufanya kazi na Trump.

"Lazima nikubali kwamba Rais wa Marekani ana mtazamo tofauti kuhusu masuala haya kuliko sisi. Lakini hilo halibadilishi ukweli kwamba bado nina imani kwamba Wamarekani ni washirika muhimu kwetu - wale muhimu zaidi katika Muungano wa Atlantiki Kaskazini. Na kwamba tuna maslahi ya pamoja katika Ulaya na Amerika kufanya kazi pamoja ili kukomesha mgogoro huu na kisha, kwa mfano, kukomesha mgogoro, vita nchini Ukraine. Kutoa dhamana ya pamoja ya usalama kwa Ukraine. Tayari tumefanikisha mengi pamoja katika suala hili."

Merz anasema hakuna uwezekano wa uwasilishaji wa makombora ya Marekani chapa Tomahawk nchini Ujerumani.
Merz anasema hakuna uwezekano wa uwasilishaji wa makombora ya Marekani chapa Tomahawk nchini Ujerumani.Picha: Thomas Ernst/ARD/dts Nachrichtenagentur/IMAGO

Merz alilengwa na Trump ambaye alimkosoa kwa kusema kwamba Iran inaiaibisha Marekani kwenye meza ya mazungumzo. Trump alimshutumu Merz kwa kufikiri ni sawa kwa Iran kuwa na silaha za nyuklia na kutoa maoni kwamba Ujerumani ilikuwa ikifanya vibaya sana, kiuchumi na vinginevyo.

Maoni ya Trump kuhusu Merz yalifuatiwa na tangazo la kupunguzwa kwa wanajeshi wa Marekani nchini Ujerumani. Siku hiyo hiyo, alitangaza ongezeko la ushuru wa magari na malori kutoka Umoja wa Ulaya, hatua ambayo ingeathiri zaidi uchumi wa Ujerumani.

Merz anafikiria nini kuhusu vita vya Iran?

Merz ndiye kiongozi wa hivi karibuni wa Ulaya kukosolewa na Trump kama hatua ya kujibu kutokubaliana kwao kuhusu vita vya Iran. Trump pia amekuwa na ugomvi na Uhispania na Uingereza kuhusu jambo hilo.

Lakini kansela Merz alisisitiza kwamba bado analiunga mkono lengo la Trump la kuhakikisha Iran haipati kamwe silaha za nyuklia, akiashiria kwamba Ujerumani bado inasimama pamoja na kuyaunga mkono maslahi ya Marekani upande huo.

Merz anasema hakuna uwezekano wa uwasilishaji wa makombora ya Tomahawk.
Merz anasema hakuna uwezekano wa uwasilishaji wa makombora ya Tomahawk.Picha: Department of Defense/ZUMA/picture alliance

Merz anasema hakuna uwezekano wa uwasilishaji wa makombora ya Tomahawk

Merz pia alionekana kuithibitishia ARD kwamba upelekaji uliopangwa wa makombora ya masafa marefu chapa Tomahawk kutoka Marekani kuja Ujerumani ungesitishwa, angalau kwa sasa.

"Kama ninavyoona kwa sasa, kusema ukweli, hakuna uwezekano wowote wa Marekani kusambaza mifumo ya silaha za aina hii," Merz alisema. "Wamarekani wenyewe hawana makombora ya kutosha kwa sasa."

Usafirishaji wa Tomahawk ulikuwa umeahidiwa na rais wa zamani wa Marekani Joe Biden, huku kukiwa na hatua nyingi zilizochukuliwa wakati huo ili kujikinga na tishio la Urusi.

Merz alisema vita nchini Iran na Ukraine vilikuwa vinaathiri usambazaji wa Marekani wa makombora ya Tomahawk, lakini alidokeza kwamba hii ilikuwa hatua ya muda mfupi na inaweza kubadilika katika siku zijazo.