Marekani kuongoza meli zilizokwama Mlango Bahari wa Hormuz
4 Mei 2026
Marekani Jumatatu itazindua operesheni ya kuongoza meli zilizokwama kutoka Mlango Bahari wa Hormuz ulioshikiliwa na Iran. Hayo yamesemwa na rais Donald Trump wa Marekani akitoa maelezo machache kuhusu juhudi kubwa za kusaidia mamia ya meli na mabaharia wapatao 20,000.
Trump alisema katika chapisho la mitandao ya kijamii Jumapili kwamba nchi zisizoegemea upande wowote na zisizo na hatia zimeathiriwa na vita vya Iran.
Trump ameziambia nchi hizo kwamba wataongoza meli zao salama kutoka kwenye njia hizo za majini zilizowekewa vikwazo ili waweze kuendelea na biashara zao na kwa urahisi.
Trump alisema operesheni maalumu iliyopewa jina "Project Freedom" itaanza leo asubuhi katika Mashariki ya Kati, akiongeza kuwa wawakilishi wake wanafanya mazungumzo na Iran ambayo yanaweza kuleta tija na kusababisha jambo chanya sana kwa wote.