1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Merz: CDU imeibuka kuwa imara katika uchaguzi wa NRW

15 Septemba 2025

Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz, amekaribisha matokeo ya mwanzo ya uchaguzi wa serikali za mitaa katika jimbo la North Rhine-Westphalia, unaokipa ushindi chama chake cha Christian Democratic Union, CDU.

https://p.dw.com/p/50VaV
Berlin 2025 | Friedrich Merz
Kansela wa Ujerumani Friedrich MerzPicha: Christophe Gateau/dpa/picture alliance

Ushindi huo unatokea wakati chama kinachofuata siasa kali za mrengo wa kulia, AfD, kikiongeza umaarufu wake kwa asilimia 5 ikilinganishwa na uchaguzi uliopita wa mwaka 2020.

Merz aliyeigia madarakani mwezi Mei na ambaye chama chake kimetabiriwa kuongoza kwa asilimia 33.3  amesema chama chake kimeibuka kuwa imara kwa kutatua matatizo ya wajerumani hasa katika uchumi, uhamiaji, na usalama.

Uchaguzi huyo ni kipimo cha kwanza debeni kwa serikali ya muungano ya Kansela Merz inaojumuisha muungano wa kihafidhina wa vyama vya Christian Democratic Union, CDU, na Christian Social Union, CSU, na Chama cha siasa za wastani zinazoegemea mrengo wa kushoto cha SPD.