Mazungumzo ya Annapolis kuhusu mashariki ya kati | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 26.11.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Mazungumzo ya Annapolis kuhusu mashariki ya kati

Israel na Wapalestina kujadili masuala tete katika mgogoro huo ikiwa ni pamoja na haki ya kurejea wakimbizi wa kipalestina.

default

Waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert na mkewe Aliza walipowasuili Annapolis jana(Jumapili)

Rais George W.Bush wa Marekani anakutana na viongozi wa Israel na Palestina leo katika jaribio la mwisho la kulipa msukumo suala la kuundwa dola ya Palestina, kabla hakumaliza muda wake wa madaraka ikisalia miezi 14.

Pamoja na hayo wadadisi wanasema matarajio ni finyu katika mazungumzo hayo ya siku tatu huko Annapolis karibu na mji mkuu Washington.

Kukusokana kwa matarajio makubwa katika mazungumzo hayo kutnatokana na ile hali ya kwamba Bush, Waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert na rais wa Palestina Mahmoud Abbas-wote wanakabiliwa na changamoto ya kisiasa nyumbani.

Hata hivyo katika kile kinachoonekana kuwapa motisha viongozi wote hao watatu, Syria na Saudi Arabia zimeahidi kuhudhuria mkutano wenyewe hapo kesho, ingawa Syria itawakilishwa na waziri mdogo badala ya waziri wake wa mambo ya nchi za nje.

Marekani inasema kazi ngumu zaidi itaanza baadae, wakati pande zote mbili zitakapoanza kuyajadili masauala ya msingi ya mgogoro wao- haki ya wakimbizi wa kipalestina, hatima ya mji wa Jerusalem, usalama na mipaka ya Palestina ya siku zijazo.

Akizungumza na waandishi habari afisa wa ngazi ya juu katika ujumbe wa Palestina Saeb Erekat alisema,“Tuko hapa na mataifa 49 na anafikiri ni juu yetu sisi na Waisraili kuchukua maamuzi yanayofaa kwa ajili ya amani.”

Ujerumani inawakilishwa katika mazungumzo hayo na Waziri wa mambo ya nchi za nje Frank-Walter Steinmeier.

Mkutano huo wa Annapolis huko Maryland unafuatia kushindwa kwa miaka kadhaa kwa utawala wa rais Bush kuupa umuhimu mkubwa mgogoro huo, kinyume na mtangulizi wake Bill Clinton.

Mshauri wa usalama katika ikulu ya Marekani Stephen Hadley amesema anazitarajia pande zote mbili kuupa zingatio jipya mpango wa ramani kuelekea suluhisho la mzozo huo uliozinduliwa 2003, ambao ni pamoja na suala la kusitishwa makaazi ya Wayahudi katika ukingo wa magharibi na Wapalestina kupambana na wanaharakati.

Marekani inahoji kwamba wakati ni muwafaka kwa mazungumzo licha ya changamoto inayowakabili wahusika. Sambamba na hayo pande hizo mbili zinatarajiwa kukubaliana juu ya waraka wa pamoja utakaowasilishwa katika mkutano huo.

Katika kujaribu kufanikisha hayo, Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Condoleezza Rice aliwaalika kwa chakula cha usiku jana Waziri wa nje wa Israel Tzipi Livni na kiongozi wa ngazi ya juu wa Kipalestina katika mazungumzo hayo Ahmed Qurei.

Rais Bush ambaye kisiasa amedhoofika kutokana na vita vya Iraq, atamaliza kipindi chake cha madaraka Januari 2009.

 • Tarehe 26.11.2007
 • Mwandishi Mohammed Abdul-Rahman
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CTBm
 • Tarehe 26.11.2007
 • Mwandishi Mohammed Abdul-Rahman
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CTBm

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com