Mauwaji ya Dendermonde Ubeligiji | Habari za Ulimwengu | DW | 24.01.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Mauwaji ya Dendermonde Ubeligiji

kijana aliyeuwa akabiliwa na mashtaka

Brussels:


Mwendesha mashtaka wa Dendermonde nchini Ubeligiji ameamuru atiwe korokoroni kijana mwenye umri wa miaka 20 aliyemwaga damu katika shule moja ya chekechea katika mji huo.Kijana huyo anakabiliwa na mashtaka ya kuwauwa watu watatu na kufanya majaribio kadhaa ya kutaka kuuwa.Mtuhumiwa huyo amewachoma visu watoto wawili wadogo na mlezi wao.Kijana huyo amekataa hapo awali kusema chochote kuhusu mauwaji hayo.Kwa mujibu wa maafisa wa polisi,kijana huyo alikua na akili zake,hakuwa amelewa wala kuvuta bangi alipoivamia shule hiyo ya chekecheya na kuanza kuchoma watu visu.

 • Tarehe 24.01.2009
 • Mwandishi Oumilkher Hamidou
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GfLF
 • Tarehe 24.01.2009
 • Mwandishi Oumilkher Hamidou
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/GfLF
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com