Matokeo ya wiki | Michezo | DW | 15.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Matokeo ya wiki

Timu kadhaa za afrika zarudi uwanjani mwishoni mwa wiki hii kuania tiketi zao za finali ya Kombe la Afrika nchini Ghana Januari mwakani.Kamerun na Morocco zitazamiwa kuwa zakwanza kutia mfukoni tiketi za Ghana.

Timu ya mchanganyiko ya Afrika itacheza na ile ya dunia mwezi ujao kusherehekea siku ya kutimia miaka 89 kuzaliwa mzee Nelson Mandela.

Wakati Taifa Stars ya Tanzania ime,kuwa na miadi leo na Burkina Faso huko Ouagadogou, macho ya waafrika mashariki na hasa ya waganda yanakodolewa changamoto ya kesho kati ya Uganda na Lesotho –tunazungumza na muandishi habari wa Uganda Omar mutasa juu ya matumaini ya waganda kutamba kesho baada ya kuitimua Nigeria 2:1 mjini Kampala.

Na Kenya Taifa Stars ilijiwinda vipi mwishoni mwa wiki iliopita kwa changamoto ya Kombe hili kwa mpambano wake ?

Katika ringi ya mabondia bingwa wa zamani wa wezani wa juu Vitali Klitschko atarejea ringini kupambana na Jameel McCline huko Munich,septemba 22.

Baada ya changamoto za mwishoni mwa wiki hii za kuania tiketi za finali ya kombe lijalo la Afrika la mataifa nchini Ghana ,timu za kwanza zilizotazamiwa kutoroka na tiketi zao zilikuwa samba wa nyika Kamerun na samba wa Atlas Morocco.Pia ushindi kwa Algeria na Angola ulitazamiwa kuwahakikishia nafasi zao huko Ghana hapo Kati ya Januari hadi februari.

Timu nyengine kabla firimbi kulia leo jumamosi zilizotazamiwa kujiunga na hizo ni Tembo wa Ivory Coast,Super Eagles wa Nigeria,Tunisia na Senegal na hata Togo na Afrika kusini.hii ikitegemea matokeo ya mwisho ya changamoto za mwishoni mwa wiki hii.

Macho ya waganda yanakodolewa kesho Lesotho ambako baada ya kupiga kambi Afrika Kusini,Ugandan cranes wamenoa makucha yao kuwatia mwereka walesotho kama walivyowafanyia wanigeria.

Senegal iliodhofika na sio ile timu iliotia for a hadi robo-finali ya kombe la dunia 2002 ikitarajiwsa kunyakua tiketi yake leo ya accra kutoka kundi la 7 mradi tu itambe mjini Maputo, mbele ya Msumbiji na Burkina Faso na Taifa Stars Tanzania zitoke suluhu mjini Ouagadogou:

Shabiki mmoja wa Tanzania alibashiri kuwa Burkina Faso ingewika nyumbani kwani timu zote katika kundi hili zimetamba nyumbani.George njogopa alitufungulia pazia la changamoto ya leo kabla firimbi kulia huko Ouagadogou:

Kenya Harambee Stars ilijipima nguvu na Rwanda huko Kasarani mwishoni mwa wiki iliopita huku timu zote mbili zikijinoa kwa changamoto zao za mwishoni mwa wiki hii:

Duru za mwisho za kuakata tiketi za Ghana zitakua mapema septemba na Oktoba 20 itapigwa kura kuyagawanya makundi 4 kutoka timu 16 zitakazoumana mjini Accra.

Nje ya kinyan’ganyiro cha kombe la Afrika ,imetangazwa mjini Cape Town kuwa mpambano maalumu umeandaliwa kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mzee Nelson Mandela.Timu ya Afrika itacheza nay a dunia kuadhimisha mwaka wa 89 wa kuzaliwa kwa mzee Mandela.

Mwenyekiti wa Kamati ya maandalio ya kombe la dunia 2010 Danny Jordaan ameliambia jukwaa la uchumi la afrika juzi kuwa rais wa FIFA Sepp Blatter atahudhuria mechi hiyo.Blatter atakuwa nchini Afrika Kusini hapo juni 18 na 19 na ataonana na rais Thabo Mbeki.

Kesho Real Madrid ya Spain imepania kuivua taji FC Barcelona mradi tu inaichapa Real Mallorca.Real ilipigania Robinho aruhusiwe kuwa uwanjani badala ya kujiunga na kikosi cha Brazil kwa Copa America.FIFA iliridhia ombi la Real.Endapo Real ikiishinda Mallorca na kutwaa taji,hiyo itakua zawado nono kwa David Beckham alieshadidia kuiacha mkono na kujiunga msimu ujao na Los Angeley Galaxy.

Katika ringi ya mabondia,bingwa wa zamani wa wezani wa juu duniani,muukrain aliepiga kambi yake Ujerumani-Vitali klitschko atarejea ringini kutwangana ndondi mjini Munich na muamerika Jameel McCline.Miadi yao imewekwa septemba 22.Changamoto iliopangwa dhidi ya bingwa wa taji la dunia la WBC mrusi Oleg Maskaev mjini Moscow, Juni 2 umevunjika.Klitschko alikuwa na rekodi ya kushinda mapambano 342 na kushindwa 2 alipotangaza kujiuzulu.Nduguye mdogo Wladmir klitschko ndie bingwa wa shirika la IBF wa taji la dunia la wezani wa juu.