Matokeo ya Kura ya Maoni Visiwani Zanzibar
2 Agosti 2010Matangazo
Hiyo ina maana Baraza la Wawakilishi visiwani humo litakutana kuibadilisha katiba ya Zanzibar ili kuweka njia wazi ya kuweko serikali ya Umoja wa taifa, huenda sana baina ya vyama vya CCM na CUF.
Othman Miraji alizungumza punde hivi na mkuu wa upinzani katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hamad Mohammed, ambaye yumo katika uongozi wa Chama cha CUF, na pia Othman Miraji alizungumza na Harun Suleiman, waziri wa elimu wa Zanzibar, na mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama tawala cha CCM.