MASHARIKI YA KATI | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 16.03.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

MASHARIKI YA KATI

Wapalestina waitisha siku ya "ghadhabu" kuania Jeruselem

Biden (Marekani) na Netanyahu (israel)

Biden (Marekani) na Netanyahu (israel)

Maalfu ya wapalestina, wameandamana hii leo katika mitaa ya Mwambao wa Gaza siku ya "Ghadhabu" iliotangazwa na chama cha HAMAS ili kulalamika dhidi ya kufufuliwa kwa Synagogi (msikiti wa wayahudi) lililojengwa karne ya 17 mjini Jeruselem.Wapalestina kadhaa walipambana na polisi wa Israel.

Waziri-mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu jana alikataa mpango wowote wa kuzuwia ujenzi wa maskani za walowezi wa kiyahudi ndani na katika vitongoji vya jiji la Jeruselem.Hivyo, ameonesha kuendelea kutojali ila zilizotolewa na mshirika wake wa chanda na pete-Marekani juu ya ujenzi wa maskani hizo.Nae mwakilishi wa siasa za nje wa Umoja wa Ulaya,Bibi Catherine Ashton,anazitembelea nchi za kiarabu kama Misri,Jordan,Lebanon na Syria kabla ya mkutano wa pande 4 juu ya Mashariki ya Kati mjini Moscow.

MAANDAMANO:

Wpalestina hao wakipaza sauti kusema, "Kwa damu yetu,kwa moyo wetu,tunajitoa mhanga kwa ajili yako-mji wa Jeruselem." Kundi hilo la maalfu likijumuisha zaidi wanafunzi , likipepea bendera za wapalestina.Maandamano hayo yamefanyika katika miji mbali mbali ya Mwambao wa Gaza,pamoja nayo Jabaliya,Beit Lahiya,Khan Yunis na Rafah.

Mjini Gaza,waandamanaji hayo katika siku hii ya "Hasira" iliotangazwa na chama cha Hamas ,walikuwa wakusanyike nje ya Bunge la Palestina,lililohujumiwa kwa mabomu na Israel ,wakati wa mashambulio yake makubwa huko Gaza, Desemba mwaka juzi 2008-hadi Januari, 2009.

HOFU ZA WAPLESTINA:

Wapalestina, wanahofia kuwa, kufunguliwa upya kwa synagogi hilo, ni hatua ya kwanza katika mpango wa Israel, wa kuubomoa kabisa msikiti wa Al-Aqsa na kulijenga upya sinagogi hilo l lililobomoka.Sinagogi hilo, ni kituo pia kitakatifu kwa wayahudi wanaokiita "Temple Mopunt" kwavile , ni mahala pa kituo chao cha pili kitakatifu kilicho teketezwa na warumi mwaka 70 AD.

Machafuko haya kati ya wapalestina na polisi ya Israel, ni changamoto nyengine katika juhudi za Marekani, kuyafufua mazungumo ya Mashariki ya kati baada ya Israel kuwakasirisha wapalestina kwa kutangaza kujenga majumba 1.600 kwa walowezi wa kiyahudi katika ardhi zao huko Mashariki mwa Jeruselem.

Waziri-mkuu Netanyahu, jana tu alipinga vizuwizi vyovyote vya ujenzi wa maskani za wayahudi ndani na kandoni mwa Jeruselem.Hivyo, anaendelea kubisha dai la mshirika wake Marekani.Marekani imelaani mpango wa Israel wa kujenga majumba 1.600 mapya huko Ramat Shlomo.

BIBI HILLARY CLINTON:

Vyombo vya habari vya Israel, vimearifu kuwa, waziri wa nje wa Marekani bibi Hillary Clinton,aliitaka Israel wiki iliopita, ifute kabisa mpango wake huo.Wachunguzi wanahisi, uamuzi wa waziri mkuu Netanyahu kutojali dai hilo, unabainisha kuwa anaungwamkono vya kutosha nchini Israel ili kuzima vishindo kutoka Washington.

Nae mwakilishi wa siasa za nje wa Umoja wa Ulaya, Bibi Catherine , Ashton,akizuru wakati huu nchi za kiarabu kabla ya ule mkutano wa pande 4 mjini Moscow, juu ya Mashariki ya Kati,alisema huko Cairo, kuwa kuna haja ya kufanywa haraka mazungumzo kati ya Israel na wapalestina.

Mwandishi: Ramadhan Ali/RTRE

Uhariri : M.Abdul-Rahman

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com