1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaRwanda

Marekani yazionya Rwanda na Kongo kujiepusha na vita

Saumu Mwasimba
21 Februari 2024

Marekani imezionya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ikisema nchi hizo zinapaswa kujiepusha kutumbukia kwenye vita.

https://p.dw.com/p/4cfyZ
Kongo I Kanali John Imani Nzenze, mwakilishi wa kundi la waasi wa M23
Kanali John Imani Nzenze, mwakilishi wa kundi la waasi wa M23Picha: Guerchom Ndebo/AFP

Kauli ya Marekani imetolewa na mjumbe wake katika Umoja wa Mataifa kwenye mkutano wa dharura uliofanyika kuhusu Kongo.

Kongo, Umoja wa Mataifa na nchi za Magharibi wanaituhumu Rwanda kwamba inaliunga mkono kundi la waasi linaloendesha hujuma zake Mashariki mwa Kongo, kwa lengo la kutaka kudhibiti sehemu kubwa ya rasilimali ya madini katika eneo hilo.

Rwanda hata hivyo inakanusha madai hayo.

Vita vimechachamaa katika eneo la karibu na mji wa Goma tangu mwezi uliopita baada ya kushuhudiwa miezi kadhaa ya utulivu kiasi.