1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yabadili mkakati wake kuhusu Irak:

14 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CEDe
WASHINGTON: Kutokana na kuzidi kuhujumiwa askari wake wa kijeshi na muungano wa vikosi, Marekani inabadili mkondo wa siasa yake mkabala wa Irak. Rais George W Bush ameammuru gavana wa kimarekani nchini Irak, Paul Bremer, autengeneze mpango wa kukabidhi haraka madaraka kwa wananchi wa Irak. Mshauri wa masuala ya usalama wa kitaifa, Condoleeza Rice, alitamka Ikulu mjini Washington haisisitizi tena kukabidhi madaraka kufuatia kukubaliwa katiba ya Irak. Kwa mujibu wa kauli ya rais George W Bush, majeshi ya kimarekani hayataondoka Irak na Afghanistan hadi wapatikane Saddam Hussein na Osama bin Laden. Hii ni ripoti ya gazeti Fanancial Times la Ujerumani. Wakati akihojiwa, Bush alitamka wataondoa huko iwapo kazi imekamilika na juma lijalo atakuwa na ziara nchini Uingereza.