1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Marekani, Uingereza zawashambulia Wahouthi huko Yemen

Sylvia Mwehozi
25 Februari 2024

Vikosi vya Marekani na Uingereza vimefanya mashambulizi mapya dhidi ya maeneo 18 ya waasi wa Kihouthi nchini Yemen.Marekani na Uingereza zimesema mashambulizi yalilenga hasa maghala ya silaha na ndege zisizo na rubani.

https://p.dw.com/p/4crAP
Bahari ya Shamu
Walinzi wa pwani wa Marekani wakiwa wamekamata meli ya silaha ya Wahouthi kwenye Bahari ya ShamuPicha: CENTCOM/Anadolu/picture alliance

Vikosi vya Marekani na Uingereza vimefanya mashambulizi mapya dhidi ya maeneo 18 ya waasi wa Kihouthi nchini Yemen. Hayo yanajiri ikiwa ni wiki kadhaa baada ya mashambulizi dhidi ya meli zinazosafirisha mizigo katika Bahari ya Shamu yaliyofanywa na waasi hao wanaoungwa mkono na Iran.

Soma: EU yazindua operesheni ya ulinzi katika Bahari ya Shamu

Katika kauli ya pamoja, Marekani na Uingereza zimesema mashambulizi yalilenga hasa maghala ya silaha, ndege zisizo na rubani zinazotumiwa kushambulia, mifumo ya ulinzi wa anga, rada na helikopta.

Katika kauli iliyotolewa tofauti na tamko la pamoja, Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin amesema nchi yake haitasita kuchukua hatua kuyalinda maisha na uhuru wa kibiashara katika moja ya njia muhimu za usafirishaji mizigo duniani.

Lakini kundi hilo la Wahouthi nalo limeapa kuwa litapambana na mashambulizi hayo ya Marekani na Uingereza.