Maonyesho ya kibiashara yafunguliwa Hnnover | Habari za Ulimwengu | DW | 21.04.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Maonyesho ya kibiashara yafunguliwa Hnnover

-

HANNOVER

Kansela Angela Merkel ameyafungua maonyesho ya kibiashara yanayofanyika kila mwaka mjini Hannover akiwaonya wajerumani kutopoteza imani na soko lao la ndani la kiuchumi ambalo kwa miongo limekuwa likiendelea kudumisha usawa licha ya kuwepo ushindani wa masoko.Maonyesho ya mwaka huu ambayo yatachukua siku tano yanaiangazia Japan kama mgeni pamoja na kumulikia technologia ya kuhifadhi nishati.Onyo la Kansela Merkel lakuwataka wajerumani kuwa na imani na uchumi wao limekuja baada ya kuchapishwa wiki iliyopita uchunguzi wa kulinganisha mataifa matano ya Umoja wa Ulaya kuonyesha kwamba Ujerumani ina idadi ya zaidi ya watu millioni 6 wanaopokea kiwango cha chini cha mshahara hii ikiwa ni sawa na asilimia 22 ya watu wanaofanya kazi nchini humo.Wakati huohuo chama cha wafanyikazi ujerumani Verdi kimeionya kampuni ya posta ya Deutche Post kwamba huenda ikakabiliwa na migomo isiyona mwisho kuanzia mei 2 baada ya kuvunjika mazungumzo kati ya chama hicho na kampuni hiyo mjini Dusseldorf.chama cha Vedri kinataka wafanyikazi wa kampuni hiyo waongezewe mshahara kwa asilimia 7. wakati kampuni imependekeza kuongeza mshahara kwa asilimia 5.5 katika kipindi cha zaidi ya miaka miwili lakini muda wa kufanya kazi utaongezwa pia.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com