Maoni ya wahariri. | Magazetini | DW | 27.05.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Magazetini

Maoni ya wahariri.

Chama cha SPD chamteua profesa Gesine Schwan kugombea urais wa Ujerumani.

Profesa Gesine Schwan-mjumbe wa chama cha SPD katika uchaguzi wa rais nchini Ujerumani.

Profesa Gesine Schwan-mjumbe wa chama cha SPD katika uchaguzi wa rais nchini Ujerumani.

Katika maoni yao wahariri wa magazeti karibu yote ya Ujerumani leo wanazungumzia juu ya uamuzi wa chama cha Social Demokratik SPD kumteua mjumbe wake kugombea wadhifa wa rais nchini Ujerumani.

Gazeti la Hannoversche Allgemeine pia linazungumzia juu ya uamuzi wa chama cha social demokratik SPD ambacho pia kimo katika serikali ya mseto, wa kumteua mjumbe wake prof. Gesine Schwan kugombea wadhifa wa rais, na hivyo kupambana na rais wa sasa Horst Köhler -mwanachama wa chama cha CDU kinachoongoza serikali ya mseto ya Ujerumani

Rais huyo wa sasa anawania kipindi cha pili.

Gazeti la Hannoversche Allgemeine linasema chama cha SPD kimecheza mchezo wa patapotea kwa kupitisha uamuzi huo.

Mhariri wa gazeti hilo anasema wasiwasi uloikuwapo ni kwamba huenda chama hicho mwishowe kikafutu msimamao wa wananchi. Gazeti linatamka kuwa idadi kubwa ya wananchi wa Ujerumani wanataka rais wa sasa Horst Köhler aendelee na kipindi cha pili. Sababu ni kwamba hadi sasa Horst Köhler ameiwakilisha Ujerumani vizuri sana.

Gazeti la Südkurie linatilia maanani kuwa hii ni mara ya pili kwa mjumbe huyo wa SPD profesa Gesine Schwan kujaribu kuwania wadhifa huo.

Hoja iliyopo ni kwamba ikiwa chama cha CDU kina Kansela mwanamke basi chama cha SPD nacho kinastahili kuwa na mjumbe wake mwanamke kama rais wa chini. Lakini katika hayo chama hicho kinakabiliwa na mtanziko mkubwa.

Mjumbe wake hatawaweza kumshinda rais wa sasa bila ya msaada wa kura za chama cha mlengo wa shoto.

Na hakika ni vigumu sana kwa mwenyekiti wa chama cha SPD bwana Kurt Beck kuwaeleza wapiga kura juu ya uhusiano wa chama chake na chama cha mlengo wa shoto, yaani wakomunisti wa zamani.Na gazeti jingine, Braunschweig Zeitung linasema chama cha SPD kinaweza kujaribu kuligeuza suala hilo, ndani nje, au juu chini lakini ukweli utabaki palepale Chama hicho kimetoa ishara ya kuelekea mlengo wa shoto.

Hatahivyo mhariri wa gazeti la Saarbrücker anesema ni haki ya chama cha SPD kuwa na mjumbe wake katika uchaguzi wa rais.


 • Tarehe 27.05.2008
 • Mwandishi Mtullya, Abdu Said
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/E6wy
 • Tarehe 27.05.2008
 • Mwandishi Mtullya, Abdu Said
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/E6wy