Maoni ya wahariri juu ya kuishtaki Ujerumani kwa sababu ya kushiriki katika kuiokoa Ugiriki | Magazetini | DW | 06.07.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Maoni ya wahariri juu ya kuishtaki Ujerumani kwa sababu ya kushiriki katika kuiokoa Ugiriki

Wanasheria, wanasiasa na wasomi waipeleka Ujerumani mahakamani!

default

Mahakimu wa Mahakama Kuu ya Katiba ya Ujerumani.

Wahariri wa magazeti leo wanazungumzia juu ya masuala mawili. Kwanza hatua ya kulifikisha mahakamani suala la mpango wa kuikoa Ugiriki. Na pili ni juu ya hatua ya Denmark ya kurudisha tena taratibu za udhibiti mipakani.
Watu mashuhuri ikiwa pamoja na wanasheria, wanasiasa na wasomi nchini Ujerumani wameishtaki serikali ya Ujerumani kwenye mahakama kuu ya katiba ,kwa sababu ya kushiriki katika mpango wa kuiokoa Ugiriki na nchi nyingine zinazokabiliwa na madeni .

Juu ya hatua iliyochukuliwa na watu hao mhariri wa gazeti la Augsburger Allgemeine anasema washika bango wa kampeni hiyo dhidi ya serikali ya Ujerumani wanaweza kusema kwamba wamepata mafanikio kutokana na ukweli kwamba malalamiko yao yanasikilizwa na mahakama kuu ya katiba ya Ujerumani. Hata hivyo watu hao wanaweka mkazo katika masuala ya kisheria tu na wanasahau umuhimu wa uchumi .

Mhariri wa gazeti la Ludwigsburger Kreiszeitung haamini iwapo watu hao watafanikiwa katika mashtaka yao dhidi ya serikali ya Ujerumani, hata hivyo mhariri huyo anaeleza ,ikiwa mahakama itaamua kwamba serikali ya Ujerumani imeenda kinyume na sheria kwa kushiriki katika mpango wa kuiokoa Ugiriki, bara la Ulaya litakumbwa na tetemeko lisilokuwa na mithili, kiuchumi. Ugiriki itafilisika na kusababisha masoko ya fedha yaingiwe kiherehere.

Na gazeti la Handelsblatt linasema hakuna anaeweza kuliviringisha nyuma gurudumu la historia- hata mahakama kuu ya Ujerumani haiwezi kufanya hivyo. Gazeti hilo linaeleza kwamba mustakabali wa Ulaya unategemea uthabiti wa sarafu ya Euro ,kwa hiyo mahakimu wa Ujerumani wanatambua kwa uhakika kwamba, Ujerumani haiwezi tena kurejea katika sarafu ya hapo awali ya DM. Ikiwa nchi moja iliyomo katika Umoja wa sarafu ya Euro itaanguka , basi mfumo mzima wa Euro utakuwa mashakani.

Lakini mhariri wa Münchner Merkur anasema bara la Ulaya linapaswa kutambua kwamba linakabiliwa na matatizo kwa sababu ,baadhi ya serikali zinakiuka sheria. Mhariri huyo anaifafanua hoja yake kwa kuuliza: Jee wananchi waendelee kuvumilia wakati ,serikali zao zinakiuka taratibu, ati kwa sababu tu, kuyarekebisha makosa kunaweza kusababisha madhara yasiyojulikana? Bara la Ulaya limeingia katika maafa kwa sababu ya kuzipuuza sheria zake. Jee Mahakama Kuu ya katiba ya Ujerumani inao ujasiri wa kuwarudisha viongozi katika misingi ya sheria?

Gazeti la Lausitzer Rundschau linazungumzia juu ya uamuzi wa Denmark wa kurejesha taratibu za kuidhibiti mipaka yake kuanzia jana. Gazeti hilo linasema hatua hiyo inakasirisha kwa sababu inaenda kinyume na moyo wa Umoja wa Ulaya.!

Mwandishi/Mtullya abdu/ Deutsche Zeitungen /

Mhariri/-

 • Tarehe 06.07.2011
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/11pr3
 • Tarehe 06.07.2011
 • Mwandishi Abdu Said Mtullya
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/11pr3