Manama. Wamarekani wawasaidia Wakorea ya kaskazini. | Habari za Ulimwengu | DW | 31.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Manama. Wamarekani wawasaidia Wakorea ya kaskazini.

Wanajeshi wa jeshi la majini la Marekani wamewachukua wafanyakazi wa meli ya Korea ya kaskazini ambao wamejeruhiwa kwa matibabu katika meli yao ya kijeshi baada ya Wakorea hao kushambuliwa kwa risasi na kujeruhiwa katika shambulio lililofanywa na maharamia baharini nje ya pwani ya Somalia.

Jeshi hilo la majini katika meli ya kijeshi ya USS James E. Williams waliwasaidia wafanyakazi wa meli ya Korea ya kaskazini jana Jumanne ambao walipambana na maharamia na kuchukua tena udhibiti wa meli yao ya Korea ya kaskazini katika mapigano m

akali na Wasomali hao ambao waliiteka nyara meli hiyo.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com