Mahojiano na mkuu wa majeshi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo | Matukio ya Kisiasa | DW | 26.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Mahojiano na mkuu wa majeshi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo

Nchini Kongo Kamanda mkuu wa jeshi la nchi hiyo Luteni Jen Deudeni Kayende yuko ziarani katika mkoa wa Kivu ya Kaskazini eneo la mashariki alikozuru mji wa Sake karibu na eneo la mapigano.

Kiongozi huyo wa jeshi ametangaza kuandaliwa kwa vituo maalum vya kuwapokea waasi wanaotaka kujiunga na jeshi la taifa huku mapigano yanaendelea. Majeshi ya serikali na waasi walifikia makubaliano ya kusitisha vita mwanzoni mwa mwezi huu yaliyosimamiwa na ujumbe wa Umoja wa mataifa nchini humo MONUC.

Mwandishi wetu John Kanyunyu alikuwa katika eneo la Goma na kuzungumza na kiongozi huyo wa jeshi. Anaanza na kumuuliza kwanini amewaagiza raia kurudi kwao huku waasi wakirandaranda.

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com