Mahakama ya Thailand yaivunja serikali ya Somchai S Wongsawat | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 02.12.2008
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Mahakama ya Thailand yaivunja serikali ya Somchai S Wongsawat

Mahakama kuu nchini Thailand imeamurzu kuvunjwa kwa chama kinachotawala na kumpiga marufuku waziri mkuu wa nchi hiyo Somachai Wongsawat dhidi ya kushiriki katika siasa za nchi hiyo.

default

Maafisa wa usalama nchini Thailand wakiimarisha juhudi zao katika kukabiliana na waandamanaji wa kundi la People´s Power PPP, NA na kupelekea kuvunjwa kwa serikali.Hatua hiyo inafuatia  maandamano ya ghasia yaliyokumba nchi hiyo kwa muda wa majuma kadhaa sasa, na kupelekea kufungwa kwa uwanja wa ndege wa  kimataifa wa Bangkok,huku waandamanaji hao wakiendelea kuzingira uwanja huo wa ndege katika juhudi za kuishinikiza serikali ya waziri mkuu huyo kuondoa madarakani.


 Hatua hiyo sasa imeilitumbukiza taifa hilo katika hali ngumu ya kisiasa isiyoweza kubashirika.


Uamuzi wa mahakama hiyo wa kukivunja chama tawala cha  People Power  ( PPP), ulifikiwa baada ya kubainika kuwa waziri mkuu  Somchai Wongsawat, ambaye ndie kiongozi wa chama, alihusika katika kashfa ya udanganyifu na ununuzi wa kura wakati wa uchaguzi mkuu uliopita.


 Hivyo basi waziri huyo mkuu pamoja na maafisa wengine 36 wa ngazi za juu katika chama hicho sasa wamepigwa marufuku kushiriki siasa za nchi hiyo kwa muda usiopungua miaka 5.


Kadhalika vyama vingine viwili ambavyo vimekuwa vikishirikiana na serikali ya waziri huyo mkuu, pia vimevunja  kwa kupatikana na hatia ya wizi wa kura wakati wa uchaguzi mkuu wa Disemba  2007, ambao ulikuwa wa kwanza tangu kupinduliwa kwa serikali ya waziri mkuu Thaksin Shinawatra mwaka wa 2006.


 Hii inafuatia  maandamano  ya miezi kadhaa  ya wafuasi wa kundi la Peoples Alliance for Democracy (PAD), ambayo kilele chake ulikuwa kuzingirwa kwa viwanja vinne vya ndege ikiwa ni pamoja na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bankok.


 Waandamanaji hao waliuzingira uwanja wa ndege wa Bankok, katika juhudi za kumzuia waziri huyo mkuu kurejea nyumbani kutoka ziarani nchini Peru ambako alihudhuria mkutano wa kibiashara wa viongozi kutoka eneo la Asia na Pacific.


 Akiwahutubia waandishi wa habari kutoka mjini Chiang Mai, ambako ndege iliyombeba ililazimika kutua, kukwepa  zahama ya waandamanaji hao, Somchai  mwenye umri wa miaka 61 alisema kuwa amekubali uamuzi wa mahakama wa kuivunja serikali yake.


 Somchai Wongsawat ambaye ni shemejiye aliyekuwa waziri mkuu wa nchi hiyo Thaksin Shinawatra anayeishi uhamishoni,amekuwa madarakani kwa muda wa miezi mitatu pekee,ambapo kipindi chake cha utawala kimezongwa na maandamano ya wafuasi wa kundi la PAD, wakitaka kumuodoa madarakani  kwa shtuma za ufisadi na kuwa kibaraka wa waziri mkuu wa zamani Thaksin Shinawatra.


 Zaidi ya wafanyi kazi 500  wa serikali waliochoshwa na serikali ya waziri  huyo mkuu Somchai walikusanyika nje ya mahakama kusikiza uamuzi huo uliotolewa kupitia televisheni ya taifa, baada ya maandamano ya awali kupelekea jopo la majaji kubadilisha sehemu waliokotarajiwa kutoa uamuzi huo.


Uamuzi huo umetolewa huku  wafuasi wa kundi hilo la PAD, wakiendelea na maandamano yao ya kuuzingira uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bankok, hali ambayo imekwamisha kabisha shughuli za uwanja huo kwa muda wa juma moja lililopita. Polisi wa kukabiliana na ghasia  wamelikabiliana vikali na waandamanaji hao na kusababisha kifo cha Mtu mmoja na wengine 22 kujeruhiwa katika uwanja huo wa ndege.


Kwa upande mwengine waandamaji ambao wamekuwa wakipiga kambi  kwa muda wa miezi 3 katika ofisi za waziri huyo mkuu, walianza kuondoka kutoka ofisi hizo, na kuelekea katika viwanja vya ndege ili kuungana na wenzao.


 Wakati huo mkutano mkuu wa ushirikiano wa kimaendeleo wa mataifa ya Kusini Mashariki mwa Asia ambao ulitarajiwa kuanza  kati kat

i ya mwezi huu mjini Chiang Mai, umeahirishwa hadi mwaka ujao, kufuatia kuvunjwa kwa baraza hilo la mawaziri.


 Tarehe ya kufanyika kwa mkutano huo itatangazwa baada ya mashauriano na viongozi kutoka mataifa wanachama wa shirika hilo.

 • Tarehe 02.12.2008
 • Mwandishi Eric Kalume Ponda
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/G7VH
 • Tarehe 02.12.2008
 • Mwandishi Eric Kalume Ponda
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/G7VH
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com