Mafuta yazidi kusambaa katika ghuba ya Mexico | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 01.05.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Mafuta yazidi kusambaa katika ghuba ya Mexico

Mafuta yanayovuja kutoka katika kisima cha chini ya bahari katika eneo la ghuba ya Mexico yameanza kuenea hadi ufukweni katika jimbo la Louisiana hivyo kuwa kitisho cha janga la mazingira.

default

Mafuta yanayosambaa baharini kutoka katika kisima cha mafuta cha chini ya bahari yameanza kufika ufukweni mwa pwani ya jimbo la Louisiana nchini Marekani.

Washington

Mafuta yanayovuja kutoka katika kisima kwenye eneo la ghuba ya Mexico yameanza kuenea hadi ufukweni katika jimbo la Louisiana jana na hivyo kuwa kitisho cha janga la kimazingira. Rais Barack Obama wa Marekani ametoa wito wa kufanyika uchunguzi wa kina wa janga hilo.

Siku ya Alhamisi upepo mkali kutoka kusini mashariki ulisukuma utando wa mafuta hayo hadi katika mwambao ulioko katika eneo ambalo mto Mississipi huingia baharini. Shirika la mafuta la Uingereza , BP limesema litawajibika vilivyo kutokana na kuvuja kwa mafuta hayo na litalipa fidia kwa madai yatakayotolewa kuhusiana na janga hilo. Kwa mujibu wa wataalamu, makadirio ya mwanzo ya kusafisha utando huo wa mafuta yatagharimu kati ya Dola bilioni mbili na bilioni tatu.

 • Tarehe 01.05.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/NBzF
 • Tarehe 01.05.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/NBzF

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com