MADRID:Mazungumzo ya amani huenda yakafutwa
31 Desemba 2006Matangazo
Waziri mkuu wa SpainJose Luis Rodrigeuz Zapatero amesema amenuia kuyavunja mazungumzo ya kutafuta amani na kundi la wapiganaji wa ETA.
Hii ni kufuatia mripuko wa bomu la kutegwa ndani ya gari uliotokea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Madrid.
Watu 19 walijeruhiwa kwenye tukio hilo ambalo kundi la ETA limedai kuhusika.