1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mabalozi wa Urusi wahojiwa kufuatia kifo cha Navalny

20 Februari 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Stephane Sejourné amesema nchi hiyo itamwita Balozi wa Urusi mjini Paris ili atoe maelezo kuhusu kifo cha mkosoaji Alexei Navalny aliyefariki siku ya Ijumaa akiwa gerezani.

https://p.dw.com/p/4ccFY
Maandamano ya kukosoa mauaji ya Alexei Navalny
Rais Putin adaiwa kuhusika na mauaji ya Navalny Picha: Markus Schreiber/AP/picture alliance

Jana, Ujerumani pia ilimwita balozi wa Urusi mjini Berlin kuhusu kifo hicho.

Nchi za Magharibi na wafuasi wa Navalny wanadai kuwa Rais Vladimir Putin ndiye aliyehusika na kifo cha Navalny, huku ikulu ya Kremlin ikikanusha kuhusika na kusema kwamba madai hayo ya nchi za Magharibi hayakubaliki.

EU yatafakari vikwazo vipya kufuatia kifo cha Navalny

Umoja wa Ulaya umeapa kuiwajibisha Moscow baada ya kifo cha kiongozi huyo wa upinzani na unatafakari pia vikwazo vipya kuhusiana na uvamizi wake nchini Ukraine.