Maandamano ya hali ya hewa. | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 13.12.2009
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Maandamano ya hali ya hewa.

Waandamanaji mjini Copenhagen na miji mingine ya dunia, waingia barabarani kuwashinikiza viongozi wa dunia, kuchukua hatua, Copenhagen.

default

Waandamanaji waandamana kutaka Copenhagen itoa mkataba wa haki na dhati.

Polisi katika mji mkuu wa Denmark, Copenhagen wamewakamata mamia ya waandamanaji waliofanya maandamano wakiwataka viongozi wanaohudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa wa hali ya hewa kupitisha makubaliano ya dharura ya kuhifadhi hali ya hewa. Katika miji mingi kote ulimwenguni, kulifanyika maandamano,  kuwapa changamoto viongozi zaidi ya 100 watakaokutana Copenhagen, kupata makubaliano ya haki na dhati, na pia wazisaidie kifedha nchi zinazoendelea kukabiliana na athari za ongezeko la ujoto duniani. Mjini Copenhagen, waandamanaji walivunja madirisha ya maduka na kuwasha moto barabarani, na pia kuwarushia mawe polisi. Maandamano hayo yanakuja wakati mkutano huo wa hali ya hewa unaingia wiki yake ya pili. Wajumbe katika mkutano huo bado wanazozana kuhusiana na pendekezo la kupatikana kwa mkataba wa kimataifa wa hali ya hewa.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com