LUSAKA:Zimbabwe yakataa mabadiliko ya kisiasa | Habari za Ulimwengu | DW | 16.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LUSAKA:Zimbabwe yakataa mabadiliko ya kisiasa

Zimbabwe imekataa mwito wa kufanya mageuzi ya kisiasa na pia kufanya mazungumzo na chama cha upinzani cha MDC huku ikitetea demokrasia iliyopo nchini humo. Waziri wa sheria na maswala ya bunge wa Zimbabwe Patrick Chinamasa amesema katika mkutano wa nchi wanachama wa jumuiya ya ushirikiano na maendeleo ya kusini mwa Afrika SADC unaofanyika mjini Lusaka Zambia.

Waziri huyo ameilaumu Uingereza kwa mashaka yanayoikabili Zimbabwe kwa sasa.

Mataifa wanachama wa SADC yamelaumiwa kwa kulegeza msimamo dhidi ya Zimbabwe.

Katika ufunguzi wa mkutano huo rais Levy Mwanawasa wa Zambia ambae awali aliushutumu utawala wa Zimbawe leo hii alilegeza sauti yake na kuitolea mwito Zimbabwe kutafuta utulivu ili kuiepusha nchi hiyo kurudi nyuma kimaendeleo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com