LUBUMBASH:Watu 13 wauwawa kwenye ajali ya ndege ya mizigoI | Habari za Ulimwengu | DW | 27.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LUBUMBASH:Watu 13 wauwawa kwenye ajali ya ndege ya mizigoI

Watu 13 wameuwawa na wawili kujeruhiwa kufuatia ajali ya ndege ndogo ya mizigo huko kusini mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo.Ajali hiyo ilitokea hapo jana katika eneo la Kongolo.

Kwa mujibu wa Jean Claude Kabange mkuu wa shirika la kitaifa la habari ndege hiyo ilikuwa na watu 15 wafanyikazi watatu wa ndege hiyo wakiwa raia wa Urussi na wakongomani 13.Ni watu wawili tu walionusurika.

Ndege hiyo ya Urussi aina ya Antonov ilikuwa ikitokea Goma kilomita 500 kuelekea kaskazini mashariki.

Walionusurika ni pamoja na mtoto wa miaka miwili na kijana mmoja na wako hospitali.

Maafisa wanasema huenda ndege hiyo ilikuwa ikijaribu kugeuza kurudi ilikotoka baada ya rubani kuhisi inamatatizo ya kimitambo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com