LONDON : Moto mkubwa wazuka London ya Mashariki | Habari za Ulimwengu | DW | 12.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON : Moto mkubwa wazuka London ya Mashariki

Moto mkubwa umesababisha wingu zito la moshi mweusi juu ya anga ya eneo la London ya Mashariki leo hii lakini hakuna repoti za majeruhi na polisi imesema hakuna chochote cha kudokeza kwamba tukio limesababishwa na kitu kengine ziada ya moto.

Kikosi cha zima moto cha London kimesema magari manane ya zima moto na askari 40 wa kuzima motio wamekimbizwa kwenye eneo la viwanda kulikozuka moto huo katika eneo la Stratford la London ya Mashariki.

Vyombo vya habari vya Uingereza vimeripoti kusikika kwa mripuko lakini polisi imesema hakuna dokezo linaloonyesha kwamba ni tukio la kigaidi.

Mripuko huo umetokea kwenye eneo ambalo limesafishwa kwa maandalizi ya kujenga vituo vya michezo ya Olympiki ya London ya mwaka 2012.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com