LONDON: Maelfu ya wasafiri wakwama London | Habari za Ulimwengu | DW | 22.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

LONDON: Maelfu ya wasafiri wakwama London

Maelfu ya wasafiri wamekwama katika uwanja wa ndege wa Heathrow mjini London Uingereza. Hali mbaya ya hewa imewakasirisha wasafiri hao wakiwa hawana la kufanya huku mipango yao ya likizo ikiharibiwa.

Watabiri wa hali ya hewa wanasema hali hiyo huenda iendelee hadi siku ya Krismasi Jumatatu ijayo. Shirika la ndege la British Airways limefutilia mbali safari zote za ndege nchini Uingereza lakini safari za kwenda nje zinaendelea.

Uwanja wa ndege wa Gatwick na viwanja vingine vinakabiliwa na tatizo hilo.

Shirika la British Airways limewasafirisha kwa mabasi abiria 3,000 kwenda viwanja vya ndege kaskazini mwa Uingereza. Wengine wamepelekwa mjini Paris, Ufaransa na Brussels, Ubelgiji.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com