LONDON: Abiria 1 amefariki katika ajali ya treni
24 Februari 2007Matangazo
Ajali ya treni iliyotokea kaskazini-magharibi mwa Uingereza imeua mtu 1 na wengine 22 wamejeruhiwa, 5 wakiwa katika hali mbaya.Treni hiyo iliyo ya kampuni la Virgin ilitokea London na ilikuwa ikielekea Glasgow.Ilipata ajali ilipokuwa ikisafiri mwendo wa kilomita 150 kwa saa. Mwenyekiti wa Kundi la makampuni ya Virgin, Richard Branson,amemsifu dreva wa treni na wasaidizi waliofanya kazi katika hali ngumu, kuwaokoa abiria walionasa katika mabehewa yaliopinduka.