1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LISBON: Waandamanaji wapinga mageuzi ya kiuchumi nchini Ureno

3 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCMp

Kiasi ya watu 100,000 wameandmana katika mji mkuu wa Ureno,Lisbon kupinga mageuzi ya kiuchumi yaliotangazwa na serikali ya waziri mkuu Jose Socrates.Hasa,wanapinga mpango wa kutaka kupunguza gharama za hospitali na shule.Chama cha wafanyakazi cha CGTP kimeonya kuwa mipango hiyo inapuuza mahitaji ya umma.Hayo ni maandamano makubwa kabisa kupata kufanywa nchini humo katika miaka ya hivi karibuni.