1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LISBON : Leo ni siku dhidi ya hukumu ya kifo

10 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Gt

Ulaya leo inaadhimisha kwa mara ya kwanza siku dhidi ya hukumu ya kifo duniani.

Maafisa wanaokutana nchini Ureno wanashinikiza kuongezwa kwa juhudi za kidiplomasia kupiga marufuku adhabu ya kifo duniani kote.Umoja wa Ulaya pia umeitaka Marekani kuiga mfano wake katika kupiga marufuku hukumu ya kifo.

Nchi 69 duniani bado zina hukumu ya kifo kwenye vitabu vyao vya kisheria na mwaka jana takriban watu 1,591 walinyongwa.

China ina idadi kubwa ya watu hao walionyongwa ambapo takwimu rasmi zinaonyesha watu 1,000 wamenyongwa nchini humo.