1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rajaonarimampianina adai kura zimeibiwa Madagascar

Saumu Mwasimba
9 Novemba 2018

Wananchi wa Madagascar wasubiri matokeo ya uchaguzi huku tayari baadhi ya wagombea wakianza kulalamikia wizi wa kura: DRC yaendelea na mchakato wa kuwaandikissha wasimamizi,wa uchaguzi ,waandishi habari na wajumbe wa mashirika kutoka nje kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Desemba 23 huku wapinzani wakitafuta mgombea mmoja

https://p.dw.com/p/37xnn

Miongoni mwa yaliyoripotiwa  barani Afrika wiki hii  ni msako dhidi ya mashoga jijini Daresalam huko  Tanzania,Marekani ilitowa tahadhari kwa raia wake walioko katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki  huku mashirika mbali mbali ya kutetea haki za binaadamu yakilaani hatua ya kuwaandama mashoga iliyotangazwa katika jiji la Daresalam na mkuu wa mkoa huo,Paul Makonda.Nchini DRC mchakato wa kumchagua mgombea mmoja atakayepeperusha bendera ya upinzani katika uchaguzi wa desemba ndiyo iliyokuwa habari kubwa,wakati kisiwani Madagascar nako taharuki imetanda matokeo ya uchaguzi yakisubiriwa.