1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Korea Kaskazini imefanya jaribio la makombora mengi

Sudi Mnette
14 Februari 2024

Jeshi la Korea Kusini limesema limebaini Korea Kaskazini kufyatua makombora mengi baharini katika eneo lake la pwani ya kaskazini mashariki ikiwa jaribio lake la tano la silaha hizo tangu Januari.

https://p.dw.com/p/4cN2t
Korea Kusini Seoul 2024 | Jaribio la kombora la Korea Kaskazini kwenye TV
Televisheni inaonyesha picha ya kombora la Korea Kaskazinihuko Seoul, Korea Kusini, Ijumaa, Februari 2, 2024.Picha: Ahn Young-joon/AP Photo/picture alliance

Hata hivyo jeshi la Korea Kusini halikuweza kutoa idadi ya makombora yaliofyatuliwa na jinisi yalivyoruka. Zoezi hilo ni la sita kufanyika kwa mwaka huu, ikijumuishwa na Januari. Mvutano katika eneo la Rasi ya Korea kwa sasa umefikia katika kiwango cha juu zaidi katika miaka kadhaa, na hasa baada ya Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un kuongeza kasi ya majaribio ya silaha zake, na kutoa vitisho vya mzozo wa nyuklia kwa Korea Kusini na Marekani.