Kombora laharibu ′ngome′ ya waTaliban | Habari za Ulimwengu | DW | 29.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Kombora laharibu 'ngome' ya waTaliban

ISLAMABAD:

Kombora moja limeharibu maficho ya wapiganaji wa kiisalamu katika eneo la kaskazini magharibi mwa Pakistan.Maafisa wa kijasusi wanasema kuwa pia wameuawa watu 12 waliokuwa ndani mwa maficho hayo.Duru za kijasusi zinasema waliofariki ni wafuasi wa waTaliban.Hata hivyo wakazi wa eneo hilo wanasema kuwa wahanga walikuwa ni watu wa kawaida waliokuwa wanaishi katika nyumba hiyo ilioshambuliwa na kombora.Haijulikani nani aliefyatua kombora hilo.Lakini hujuma kadhaa katika eneo hilo zimekuwa zikifanywa na vikosi vya ushirika vikiongozwa na Marekani kutoka upande wa mpaka wa Afghanistan.Shambulio lililofanywa na ndege za kijeshi lilitokea usiku wa manane na lilitokea katika kijiji kimoja kilichoko katika mkoa wa Waziristani kaskazini.Eneo hilo linapakana na Afghanistan.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com