KISUMU:Ajali ya basi na lori yaua 20 | Habari za Ulimwengu | DW | 29.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KISUMU:Ajali ya basi na lori yaua 20

Watu 20 wampoteza maisha yao na wengine kadhaa kujeruhiwa pale lori lilipogongana na basi moja la abiria katika eneo la magharibi mwa Kenya.Kulingana na polisi watu 13 walikufa papo hapo baada ya lori hilo kukosa breki na kugongana na basi mjini Yala.

Watu watano walipoteza maisha yao walipokuwa wakipelekwa hospitali na wengine wawili kufariki hospitali kwa mujibu wa kamanda wa polisi katiak eneo hilo Humphrey Wanzala.Majeruhi wanapata matibabu katika hospitali zilizo karibu vilevile mjini Kisumu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com